Thursday, May 23, 2013

AINEA KATIKA MIKOA YA MWANZA NA DODOMA

AINEA
Mwanamuziki wa kizazi kipya Ainea Emmanuel au AINEA kama ajulikanavyo na wengi, yuko safarini katika ziara zake za kimuziki ambapo anatembelea mikoa ya Mwanza na Dodoma.
Ainea ambaye kwa sasa anatamba na kibao cha SOME BODY akishirikiana na Shetta anatarajia kurudi jijini Dar baadaya wiki mbili au tatu baada ya kumaliza ziara zake hizo.

ISAYA MSANGI - SHETANI IMEKULA KWAKO

ISAYA MSANGI
Muimbaji wa Nyimbo za Injili Isaya Msangi (mweye kofia) akifuatilia muimbaji mwenzake akiimba ndani ya studio za ECK PRODUCTION. Isaya Msangi ametamba sana na kibao kiulikanacho kama SHETANI IMEKULA KWAKO

Saturday, April 13, 2013

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUTOKA CONGO, FARAJA NTABOBA

FARAJA NTABOBA NA PRODUCER BENJA
Mwimbaji wa nyimbo za injili Faraja Ntaboba kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, bado yuko nchini, toka alipomaliza Show ya pasaka iliyokuwa imeandaliwa na kampuni ya Msama Promotion.
Ntaboba bado yuko nchini kwa vile bado yuko katika uandaaji wa albumu yake ya 3 ambayo inaadaliwa ndani ya Studio za Eck Production chini ya maproducer mahili kama Eck na Benja.
Ntaboba amesema hawezi kuondoka hapa nchini Tanzania mpaka akamilishe album yake hiyo ikiwa ni pamoja na kutengeneza wa video ya wimbo mmoja ambao anataka auachie kwenye vituo vya redio na tv.
Ntaboba amesema kwamba karibia ulbum zake zote anapenda kuzifanyia hapa nchini Tanzania kwa vile anaamini kuwa Maproducer wa huku wana fanya vizuri.
picha hii inamuonesha Faraja Ntaboba (kulia) akiwa na mpiga kinadamahiri sana nchini hapa, Benja

Sunday, March 31, 2013

PRODUCER KAMETA NA ECK

Procucer na miliki wa Studio za ECK Production akiwa na Producer mwenzake ambaye ni kichwa kilichomtoa Mr. NICE, nikimaanisha Producer KAMETA. Hapa walikuwa wanakula bata katika bar ya Garden Breaze Magomeni Hospitali.
PRODUCER ECK NA KAMETA
Kama anavyokuambia kameta ni kwamba hapo walikuwa wanatoa mkosi...

MO WA MO Design

Producer wa audio na Video, MO ndani ya Studio za Eck Production.
Pia ni muandaji na mtayarishaji wa filam mbalimbali za hapa nchini. anaadika Script, anadirect filam anashoot na kuedit ni mtayarishaji mwenye vipaji vingi akiwa pia ndio mmiliki wa mtandao wa
MO Designtz.blogspot.com
MO NDANI YA STUDION ZA ECK PRODUCTION
 sasa yupo katika utegenezaji wa sinema mpya ya Mtitu chini ya kampuni ya mtitu ya 5EFFECT. Ni sinema nzuri na yenye mvuto itakayokwenda kwa Jina la OMEGA. hii inawahusisha wasanii wakali wa sinema nchini kama Irene Uwoya, Dude, Mtitu na wengine wengi...

JENNIFER MGENDI NA BONY MWAITEGE

wasanii wa nyimbo za injili wakiwa ndani ya studio za eck production kwa ajili ya kurekodi nyimbo mpya
waha ni Jeniffer Mgendi na Bonny Mwaitege
BONNY MWAITEGE - JENNIFER MGENDI NDANI YA STUNDIO ZA ECK PRODUCTION