|
FARAJA NTABOBA NA PRODUCER BENJA |
Mwimbaji wa nyimbo za injili Faraja Ntaboba kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, bado yuko nchini, toka alipomaliza Show ya pasaka iliyokuwa imeandaliwa na kampuni ya Msama Promotion.
Ntaboba bado yuko nchini kwa vile bado yuko katika uandaaji wa albumu yake ya 3 ambayo inaadaliwa ndani ya Studio za Eck Production chini ya maproducer mahili kama Eck na Benja.
Ntaboba amesema hawezi kuondoka hapa nchini Tanzania mpaka akamilishe album yake hiyo ikiwa ni pamoja na kutengeneza wa video ya wimbo mmoja ambao anataka auachie kwenye vituo vya redio na tv.
Ntaboba amesema kwamba karibia ulbum zake zote anapenda kuzifanyia hapa nchini Tanzania kwa vile anaamini kuwa Maproducer wa huku wana fanya vizuri.
picha hii inamuonesha Faraja Ntaboba (kulia) akiwa na mpiga kinadamahiri sana nchini hapa, Benja